AKUPENDAYE MIYE

Nani atayekupenda kama mimi,

Nani atakutunza nikienda?

Nani atakukumbata nikiondoka?

Natamani nimjue kabla sijaenda,

 

Nani atanipenda kabla sijaenda,

Nakusihi nijulishe,

Moyo ufurahi, nafsi yangu uihuishe,

Yupi atanipenda milele? Nakuomba unijuze,

 

Nataraji moyo unipishe,

Roho usinitishe,

Kumbukumbu vazi jema mnivike,

Hizi mbiu mbele zenyu zisifike,

Masikioni zisikike,

 

Mboni hazioni fumbo hili beberu,

Simaanishi fahamu zenyu duni, hasha, hamuoni mnachotaka,

Ndio mwanzo mnatapa,

Bila doti la khanga kizunguzungu chauzungusha upendo,

Sisemi bila pesa kuna chembechembe za pendo,

Yatutesa hili fungu lojaa magendo,

 

Babananiii 2017

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s