AFRICAN BEAUTY

There's no eye that sees me better than hers, Others have got a guilty one, Up and down as the main beat, Hand in hand with my African beauty, She's elegant smooth like jazz, The ornament to my soul food kitchen, The vintage I heart, She beautifully and it is true, Yes I know too, … Continue reading AFRICAN BEAUTY

Advertisements

Ndoa Pt. 2

  Waja wote kila rika, niwaase kwa hakika. Ndoa ni kuwajibika, na hasa kumakinika. Kuna ya kutaabika, pia ya kufurahika. Ndoa ni ibada bora, ndoa ni heshima pia.   Mtafute alo mwema, ila si mkamilifu. Muombee yalo mema, akwepe ulaanifu. Mola wetu amesema, mtafute watiifu. Ndoa ni ibada bora, ndoa ni heshima pia.   Tuwaheshimuni … Continue reading Ndoa Pt. 2

Ndoa Pt. 1

  Ningekuwa nimeoa, ni mengi ningeongea. Ningekuwa na doa, ndoa ningeikemea. Ila sasa sijaoa, wala mtoto sijalea. Sasa ndoa siitaki, msiulize kwanini.   Ni wengi huisifia, wakiingia hulia. Wakale hujivunia, wakisasa hujutia. Yanini kukimbilia, wenzangu wanaumia. Sasa ndoa siitaki, msiulize kwanini.   Ooh! kama si mwanaume, basi ndoa usiiseme. Mvulana nichutame, wenye ndoa wasimame. Sina … Continue reading Ndoa Pt. 1

NAOMBA

(photo by amkatanzania.com)   Nimechoka Uchovu Wangu Ni Mchoko Wa Moyo. Nimechoka Mateso Yanadhihaki Utayari Kumoyo. Sina Hadhi Wandani Wameniuza Kwa Choyo. Masimango Ninakula Kokoto Kibogoyo. Nina Hamu Kurudi Nyumbani Ila Bado Sipaoni. Kwa mbali Roho Inatamani Macho Yangu Yamekosa Harubini Hata Miwani. Siku Hizi Najicheka Kwa Kebehi, Nakitazama Kioo Sura Yangu Haitokei. Natamani Sana … Continue reading NAOMBA

UNIKUMBUKE

(photo: Kitenge wear on IG) Nani atayekupenda kama mimi, Nani atakutunza nikienda? Nani atakukumbata nikiondoka? Natamani nimjue kabla sijaenda, Nani atanipenda kabla sijaenda, Nakusihi nijulishe, Moyo ufurahi, nafsi yangu uihuishe, Yupi atanipenda milele? Nakuomba unijuze, Nataraji moyo unipishe, Roho usinitishe, Kumbukumbu vazi jema mnivike, Hizi mbiu mbele zenyu zisifike, Masikioni zisikike, Mboni hazioni fumbo hili … Continue reading UNIKUMBUKE

Mali Ya Urithi Haiuziki

Mali ya urithi haiuziki, Na ikiuzwa hairidhishi, Hali yangu siridhiki, Kula haipikiki, Mali ya urithi haiuziki, Na ikiuzwa hairidhishi,   Mali ya urithi haiuziki, Na ikiuzwa hairidhishi, Hali hewa si rafiki, Chumi mikiki na vizingiti, Mali ya urithi haiuziki, Na ikiuzwa haikidhiki,   Mali ya urithi haiuziki, Na ikiuzwa hauridhiki, Yako yako tu haihamishiki, Wanyoshea … Continue reading Mali Ya Urithi Haiuziki